KATIBU MKUU WA YANGA, CHARLES MKWASA.
Siku moja baada ya Shirikisho la Soka Afrika [Caf] kuchezesha droo ya Kombe la Shirikisho na Yanga kujikuta ikipangwa kukutana na Mouloudia Club d’Algeria maarufu kama MC Alger, ya Algeria, uongozi wa wawakilishi hao wa Tanzania umesema safari hii wanafuta uteja kwa timu za kiarabu.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alisema jana kuwa Watanzania wamekuwa na tatizo la kisaikolojia kwa kuamini kuwa timu za Tanzania ni vibonde kwa timu zinazotoka Falme za Kiarabu.
Mkwasa alisema mchezo huo ni mchezo kama michezo mingine ya kimataifa ambayo Yanga imecheza, lakini wanapaswa kujiweka sawa kisaikolojia ili kuweza kuitupa nje ya mashindano timu hiyo.
“Kuna kasumba ambayo inatusumbua kuwa hatuna uwezo mbele ya timu hizi za Kiarabu, kitu ambacho si cha kweli…, tutajiandaa vizuri ndani na nje ya uwanja na pia tutawaandaa kisaikolojiaa wachezaji wetu na naamini tunaweza na tuna nafasi ya kusonga mbele,” alisema Mkwasa.
Alisema Yanga ina uzoefu wa michezo mikubwa na safari hii hawatakubali kutupwa nje na Waarabu kwenye michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho.
“Kocha wetu ana uzoefu na mashindano ya kimataifa, kikubwa ni kuweka mikakati sahihi kuelekea kwenye mchezo huu na tutafanya hivyo,” aliongezea kusema Mkwasa.
Yanga itaanzia nyumbani kucheza na wapinzani wao hao kati ya Aprili 7, 8 na 9, kabla ya kurudiana nao ugenini Algeria kati ya Aprili 14,15 na 16, mwaka huu.
Endapo Yanga iliyoondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Zanaco ya Zambia, itafanikiwa kuitupa nje MC Alger, itakuwa imeingia kwenye hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo.

No comments:
Post a Comment