DAR ES SALAAM: Makubwa! Wema Isaac Sepetu amezua gumzo baada ya
kujadiliwa kwenye msikiti mmoja uliopo Mwenge jijini Dar kufuatia
mhadhiri mmoja maarufu aliyefahamika kwa jina moja la Mwaipopo kuelezea
namna mwanadada huyo alivyotoa mchango wake kumsaidia marehemu Juma
Kilowoko ‘Sajuki’ alipokuwa mgonjwa.
Akizungumza kwenye msikiti huo akiwataka Waislam wamchangie fedha kwa
ajili ya matibabu ya maradhi yanayomsumbua, mhadhiri huyo alisema kuwa
anawashangaa Waislam kutokuwa na mioyo ya kuwasaidia wenzao wanapokuwa
na matatizo wakati dini haitaki hivyo.
“Nimezunguka sana kwenye misikiti mingi lakini msaada ambao nimekuwa
nikipata kutoka kwa Waislam wenzagu haukuwa wa kuridhisha, inasikitisha
sana.
Kuna wakati yule msanii wa filamu, Sajuki alipokuwa anaumwa, akina Wema
walimchangia mapesa na akaenda kutibiwa lakini sisi tumekuwa wagumu
katika kutoa,” alisema mhadhiri huyo.
Baada ya kusema, hivyo baadhi ya watu waliokuwa msikitini hapo walianza
kunong’ona chinichini wakimjadili Wema huku wengi wakisema kuwa
inakuwaje staa huyo awe na moyo wa kutoa kushinda waumini wa Kiislam
wengine ambao wamejaliwa utajiri. “Wewe fikiria kama Wema ameweza kutoa
pesa zake nyingi tu kusaidia katika matibabu ya Sajuki kipindi kile,
Waislam kwa nini tunakuwa wagumu,” alihoji kijana mmoja aliyekuwa
msikitini hapo.
Hata hivyo, hoja ya mhadhiri huyo ambaye historia yake inaonesha alikuwa
Mkristo ni kwamba, Waislam wanatakiwa kusaidiana katika shida na raha
pamoja na kwamba alikosolewa kuwa aliyemsaidia Sajuki fedha nyingi
kipindi kile hakuwa Wema bali alikuwa ni Jacqueline Wolper.
No comments:
Post a Comment