Watu
tisa (9) wamejeruhiwa katika vurugu wakati wa kuwaondoa wafanyabiashara
wadogowadogo sehemu zisizo ruhusiwa wilayani Nyamagana, mkoani Mwanza
Taarifa
ya Kamanda wa Polisi Mkoa w Mwanza DCP Ahmed Msangi imesema kwamba
tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.03.2017 majira ya saa15:45hrs
katika mtaa wa Buhongwa Center ambapo watu tisa wakiwemo askari mgambo
wa jiji la mwanza saba (07), afisa mazingira mmoja (01) na dereva wa
jiji mmoja (01) walijeruhiwa.
Amesema
watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu mbalimbali ya miili
yao na wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa wakifanya biashara pembeni
ya barabara wakishirikiana na watu wengine waliokua wakishabikia wakati
wakiendelea na zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wadogowadogo katika
maeneo yasiyo ruhusiwa haswa kwenye hifadhi ya barabara ya mwanza kwenda
shinyanga.
Aidha,
Msangi amesema katika harakati za kudhibiti vurugu hizo askari
walifanikiwa kuwakamata watu tisa ambao inadaiwa kuwa walikuwa
wakihusika katika vurugu hizo kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi
utakapokamilika, watafikishwa mahakamani.
Majeruhi wote wapo hospitali ya mkoa ya Sekou Toure wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment