Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi, ameondolewa katika wadhifa huo na kurejeshwa jeshini.
Akithibitisha
habari hizi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu (DAS), Titus Mughuha,
amesema Kanali Mkisi alitoa taarifa za uhamisho huo katika kikao cha
Kamati ya Ulinzi na Usalama na kusema kuwa, anarejea makao makuu ya
jeshi alikokuwa awali kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
‘Ni
kweli Kanali Martin Mkisi amepata barua ya kurudi makao makuu ya jeshi,
uhamisho huo ni wa kawaida na haupaswi kuhusishwa na uzushi ama sababu
zozote,” alisema Mughuha.
Kutokana
na mabadiliko hayo, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani humo, Kanali
Marko Gaguti, atakaimu nafasi hiyo hadi uteuzi mwingine utakapofanyika
kujaza nafasi hiyo.
Kanali
Martin Mkisi amedumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi tisa,
akitokea makao makuu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), kutokana na uteuzi wa
Rais, Dk. John Magufuli kwa wakuu wa wilaya 139 alioufanya Juni, mwaka
jana.
No comments:
Post a Comment