Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema Sudan kusini iko hatarini
kuingia kwenye mauaji ya kimbari.Ripoti hii ni matokeo ya uchunguzi wa
miezi saba kuhusu masuala ya haki za binadamu nchini humo.Kumekuwepo na
shutuma za ukiukwaji wa haki za kibinadamu zinazotekelezwa na wanajeshi
wa pande zote mbili kwa kufanya vitendo vya mauaji, ubakaji na uporaji.
Watu milioni moja na nusu wameikimbia nchi hiyo kwenda nchi jirani
katika kipindi cha miaka mitatu ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na
sasa ni kwa sababu ya njaa pia, Mgogoro huu wa kisiasa umeanza kwa kasi
kugawanya jeshi katika misingi ya kikabila na maeneo ya mji wa Yei.
Wakati ,Umoja wa mataifa umeonya hatari ya kutokea mauaji ya kimbari ,Brigedia jenerali Chol Deng Chol amekanusha shutuma hizo.
''hakuna vitendo vya mauaji au ubakaji, na kama kuna mwanajeshi anafanya
hivyo napaswa kumkamata haraka sana, tunaopambana nao ni waasi hapo
ndipo mauaji hutokea, wanaonusurika hudai kuwa raia wanauawa na
wanajeshi, lakini hatuwaui raia wetu nchini mwetu''
No comments:
Post a Comment