Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana alimwaga machozi mbele ya
waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa
Kimara wakati wa ibada ya Jumapili.
Mkuu
huyo wa Mkoa ambaye alikuwa ni mmoja wa watu waliohudhuria ibada ya
siku hiyo, alijikuta akibubujikwa na machozi baada ya kupewa nafasi ya
kuwasalimia waumini wa kanisa hilo.
Kabla
ya kuanza kulia, Makonda alikuwa ametumia muda wake madhabahuni kueleza
nia yake ya kuendelea na mapambano ya dawa za kulevya jijini.
Misa
ya jana katika Usharika wa Kimara ilikuwa ni mahsusi kwa ajili ya
kuombea vyeti vya kuzaliwa, vya masomo na mikataba ya ajira kwa Wakristo
wa hapo.
Wakati
wa akitoa salamu hizo, Makonda alisema nchi kupitia Dar es Salaam
imekuwa ndiyo mlango wa kuingiza na kutoa dawa za kulevya hivyo hatoweza
kukaa kimya na kushuhudia watoto na taifa vikiangamia.
“Hizi
ni dalili kwamba kazi ninayoifanya katika ulimwengu wa roho inalipa,
hakuna aliyemcha Mungu anayeweza kuacha kusimama katika kusudi zuri
ambalo Rais wetu ametuelekeza akabaki kupiga kelele hizo ndogondogo.
“Sijui
kama unafahamu baba mchungaji wamefikia hatua ya kusema sasa hata mke
wangu si raia wa Tanzania…vita hii haipiganwi kienyeji ni lazima uwe
umekaa sawasawa,” alisema Makonda.
Alisema
historia ya vita vya dawa za kulevya haijawahi kumuacha mtu salama
ndani ya Taifa na kwamba hata sasa maswali yamekuwa mengi juu yake.
“Kila
aliye jaribu ama alikufa, alifungwa, alipata kila aina ya msukosuko na
hatimaye jambo hilo likafanya waovu, wauaji wapate mali kwa njia
isiyokuwa halali. Wakapata nguvu na kutengeneza hofu ya kwamba yeyote
yule ajaribuye kushughulika nao atashughulikiwa.
“Ndio
maana mara kadhaa nimekuwa nikisema ni lazima uwe unamjua Mungu, uwe na
uhakika na Mungu unayemwamini na kama huna uhakika usithubutu kuingia
kwenye mapambano haya,” alisema.
Aliwabeza
wanaoendelea kumjadili na kusema kuwa ukuu wa mkoa si tatizo bali hoja
ni namna gani ameitumia nafasi aliyopewa kutekeleza kusudi la Mungu hapa
duniani.
“Maswali yamekuwa mengi juu ya njia lakini unapotaka kuwavusha watu kwenda ng’ambo ya pili hakuna mjadala juu ya njia.
“Kuwa
mkuu wa mkoa si tatizo, tatizo umeikamilishaje kazi ya Mungu aliyokupa
hapa duniani, hapa tuko kwenye vita na vita hii si ya ulimwengu wa mwili
bali ni ya ulimwengu wa roho.
“Wananchi
wa wamechanganyikiwa, kila wakipita mahala wanaona watoto wanatumia
dawa za kulevya na wakiangalia nyuma wanaona wale wauzaji wakubwa
hawashikiki, wanatisha, hawajui wapite wapi,” alisema.
Alisema
Jiji la Dar es Salaam ndilo lango kuu la uchumi ambapo asilimia 80 ya
mapato yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yanatoka Dar
es Salaam. Hata hivyo limekuwa lango la uchumi mbadala wa kuingizia dawa
za kulevya na kuangamiza taifa.
“Rais
hawezi kutoa elimu bure kuanzia msingi hadi sekondari ama kuwakopesha
watoto wasome halafu wakaendelea kuvuta bangi ama kutumia dawa za
kulevya je, ni mzazi gani mwenye akili timamu atakaye furahia hilo,
kiongozi gani mwenye ufahamu wa kimungu anayefurahia hilo?
“Mcha
Mungu gani anaweza akakaa kwenye mkoa kama huu akaruhusu madawa yapite
halafu watoto wanateketea, mcha Mungu anaweza akaruhusu uovu uendelee
kutawala halafu anajiita anamtumikia Mungu?
“Mcha
Mungu gani huyo…nikisema mtamjua, sikatai dini yake na wala sitaruhusu
akatize katika anga la utawala nililopewa, nimepewa bendera ya Tanzania,
nimepewa mamlaka nina ‘operate’ kutoka kwenye mamlaka ya juu sana.
Nitasimama hadi mwisho kuhakikisha jina lipitalo majina yote
linainuliwa,” alisema Makonda huku akishangiliwa.
Mara
kwa mara katika mahubiri yake alikuwa akitoa mifano kwa kutumia baadhi
ya maneno kutoka katika kitabu cha Biblia na kushangiliwa na waumini wa
usharika huo.
“Vita
tuliyonayo ni kazi ya mauti na uzima, kuhakikisha tunamtoa mtoto fulani
kwenye makucha ya shatani na hii kazi yesu alishaifanya…ukitaka kujua
kaifanya wapi soma.
No comments:
Post a Comment