MAKAMU WA RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF), WALLACE KARIA.
MAKAMU wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema kuwa anaipa nafasi Azam FC kupata ushindi dhidi ya Mbabane Swallows na kusonga mbele katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika wanayoshiriki.
Mabingwa hao wa Kombe la Kagame, wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kuweza kusonga mbele katika michuano hiyo ya kimataifa.
Akizungumza jijini hapa jana, Karia ambaye ameambatana na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo, James Muhagama, wote kwa pamoja walisema kuwa wanakiamini kikosi cha Azam FC ambacho kitashuka uwanjani kikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 walioupata nyumbani.
Karia aliongeza kuwa ni muhimu kwa wawakilishi hao wa Tanzania kuibuka kidedea, huku akidai kuwa ina mahesabu mazuri kutokana na kuondoka na ushindi katika mchezo wa kwanza.
Karia alitoa ushauri kwa wachezaji wa timu hiyo kuzingatia nidhamu ya mchezo wakiwa uwanjani huku akiwataka wahakikishe wanapata bao mapema ili kuuweka mchezo kuwa mgumu kwa wenyeji.
“Kwa hali hiyo sisi tunauhakika kabisa Azam FC wapo katika nafasi nzuri ya kupita na mambo mengine tunamwachia Mungu, cha msingi wachezaji wa Azam FC wawe na nidhamu ya mchezo ya kujua kuwa wanacheza ugenini, Azam FC sio wageni kwenye michuano ya kimataifa, makosa waliyojifunza nyuma huko watayarekebisha ili waweze kupita,” aliongeza.
Mbabane Swallows itawakaribisha Azam FC kesho kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo, mjini Mbabane, kuanzia saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments:
Post a Comment