Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetoa tahadhari kwa
wananchi kuhusu uwepo wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos), inayotapeli
watu fedha kwa kutumia majina ya watu maarufu nchini.
Tahadhari
hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum
ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema
Saccos hiyo yenye jina maarufu la Focus Vicoba kwenye mitandao ya
kijamii kama Facebook na tovuti inayojulikana kwa jina
“http://www.vicobaloanstz. wapka-mob” www.vicobaloanstz. wapka-mob,
hutumia majina ya viongozi serikalini na watu maarufu, kwa nia ya
kuwatapeli wananchi.
Alisema
majina ya viongozi yanayotumiwa na matapeli hao ni pamoja na jina la
mke wa Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Salma Kikwete, Mbunge
wa Kawe Halima Mdee na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald
Mengi.
Aliongeza
kuwa matapeli hao, hutumika kufungua akaunti za facebook na tovuti
mbalimbali, ambazo hutumia kuwarubuni watu kwa kuwaaminisha kuwa
wanaweza kupata mikopo yenye masharti nafuu na haraka zaidi kwa njia
hiyo ya mtandao.
Alisema
katika ufuatiliaji wa suala hilo, kitengo cha upelelezi wa makosa ya
mtandao cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kimebaini kuwa katika
tovuti “http://www.vicobaloanstz. wapka-mob” www.vicobaloanstz.
wapka-mob picha na jina la Mama Salma, limetumika huku kwenye ukurasa wa
Facebook wakitumia jina la Mengi, likiwa ni pamoja na namba za simu
0757 308381 na 0768 199359 ambazo si za Mama Salma wala Mengi.
Aidha,
alisema katika ufuatiliaji wa jambo hilo, Desema 16 mwaka jana
alikamatwa mtu aliyefahamika kwa jina la Boniface Ojwando (27) baada ya
kubainika kuwa anahusika katika mtandao huo wa kujipatia pesa kwa njia
ya udanganyifu kupitia mitandao hiyo ya kijamii, ambapo mpaka sasa
mtuhumiwa ameshafikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka hayo
yanayomkabili.
“Nitoe
onyo kwa wale wote wanaondelea kufanya udanganyifu huu wa kujipatia
fedha kwa njia isiyo halali kupitia mitandao ya kijamii kuacha mara
moja, kwani sheria iko wazi na pindi watakapokamatwa, watachukuliwa
hatua kali,”alisema Sirro.
Alitoa
rai kwa wananchi wote, kutokuwa wepesi kukubali matangazo ya mikopo,
yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii, bila kufika katika ofisi husika
ili kujiridhisha kuhusu utolewaji wa mikopo hiyo, ili kuepuka
kutapeliwa fedha na mali zao.
No comments:
Post a Comment