Ushauri huo umetolewa na mbunge wa zamani wa Kikwajuni Parmukh Singh
Hoogani, alipokuwa akizungumzia hatua ya Shirika la Umeme (Tanesco),
kutoa siku 14 wadaiwa kulipa kabla ya kukata huduma wakiwamo Shirika la
Umeme Zanzibar (ZECO).
Alisema pamoja na ZECO kudaiwa na Tanesco kiasi cha Sh. bilioni 122 kama
gharama za huduma ya umeme, lakini ZECO wanastahili kulipwa gharama za
matumizi ya miundombinu ambayo imetumika kufikisha huduma hiyo.
Alisema deni la Tanesco la muda mrefu hatua ya kuunda tume itaweza
kufahamu sababu ya ZECO kushindwa kulipa gharama za huduma ya umeme
wakati wananchi wamekuwa wakilipia huduma hiyo.
“Wananchi Zanzibar tunapata huduma kwa kukopesha Shirika kwa sababu
tunalipa kabla ya kutumia kupitia mita za TUKUZA haiwezekani shirika
lishindwe kujiendesha kibiashara,” alisema Singh.
Alisema tume hiyo itaweza kuja na mapendekezo mwafaka ya kutafuta njia
mbadala ya kumaliza deni la umeme na mpango kazi wa kulisaidia shirika
kujiendesha kibiashara.
Alisema kabla ya Tanesco kukata huduma ya umeme Zanzibar, kunahitajika
hekima na busara ili kulinda siasa za Muungano na maslahi ya Zanzibar na
wananchi wake.
“Kama wananchi wa Zanzibar wanalipa huduma ya umeme tena kabla ya
kutumia kuwanyima huduma kwa sababu ya deni la Tanesco na ZECO sio
kuwatendea haki,”alisema Singh.
Alisema hivi karibuni ZECO wamefikia kufungiwa ofisi za makao makuu na
Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), kutokana na kudaiwa Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT), ambayo wamekuwa wakikusanya kama wakala wa serikali
kupitia malipo ya umeme kutoka kwa wateja wake.
Aidha, alisema wakati umefika kwa Zanzibar kwenda kujifunza kwa nchi
nyingine za visiwa zimeweza vipi kuwa na umeme wa uhakika wa kujitegemea
badala ya kutegemea chanzo kimoja cha kuzalisha umeme.
No comments:
Post a Comment