Baadhi ya Watanzania waliofukuzwa nchini Msumbiji wakionyesha hati zao za kusafiria baada ya kuwasili Mtwara jana.
Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama amesema hadi kufikia juzi, Watanzania waliojisajili katika mpaka wa Kilambo wakitokea Msumbiji walikuwa 220.
Amesema tayari watu 109 wa awamu ya kwanza wamesafirishwa, ambao waliishukuru Serikali na wakazi wa Mtwara kwa kuwapokea na kuwapa misaada mbalimbali.
Mmoja wa waliorudishwa, Mwajuma Abdallah amesema: “Tunawashukuru wanamtwara na Serikali kwa jumla kwa kutupokea vizuri leo (jana) tunarudi nyumbani.”
No comments:
Post a Comment