Serikali ya Demokrasia ya Congo imekataa wito wa kimataifa wa kulitaka taifa hilo kufanyia uchunguzi picha ya video inayowaonyesha raia wa nchi hiyo wakiwaua mwanamke na mwanaume.
Msemaji wa serikali amesema kuwa ilikuwa ni wajibu wa wanaolituhumu jeshi kuweza kutoa uthibitisho wa tuhuma hizo.
Video hiyo iliyozagaa mwishoni mwa wiki inaonekana kuwa ilichukuliwa katika mji wa Kasai jimbo la kati nchini humo,ikionyesha wanajeshi wakikabiliana na wapiganaji.
Marekani imelaumu kuhusiana na video hiyo na kusema ni ukiukaji wa haki za binadamu.
Mkuu wa idara ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa Zeid Ra'ad al Hussein anasema serikali inapaswa kuangalia kile ambacho tuhuma dhidi ya ukiukaji wa haki za bina
No comments:
Post a Comment