MSHAMBULIAJI DONALD NGOMA.
Ngoma, ambaye baada ya mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba, alikwenda kwao Zimbabwe kutokana na matatizo ya kifamilia, alirejea nchini juzi na jana alishiriki kikamilifu kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini jijini.
Muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Lwandamina alisema mchezaji huyo ameonekana yupo fiti na alishiriki kikamilifu mazoezi yote ya jana.
"Amerejea na nguvu, amefanya vizuri mazoezini," Lwandamina alisema. "Nitamuangalia kwenye mazoezi ya kesho (leo) na kuanzia hapo nitajua kama nitamtumia katika mechi ijao, ila ameonyesha kuwa na utayari wa kurejea uwanjani."
Ngoma aliumia kifundo cha mguu katika mechi yao ya hatua ya makundi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Zimamoto, majareha ambayo yalimfanya akose mechi mbili zilizofuata za Kombe la Mapinduzi walizopoteza dhidi ya Azam FC na Simba kisha akakosekana pia katika mechi mbili za Ligi Kuu walizoshinda dhidi ya Majimaji na Mwadui FC.
Wakati Ngoma akiwasili nchini na kuanza mazoezi na wenzake, beki a kati wa timu hiyo, Vincet Bossou, anatarajiwa kuwasili jijini leo.
Awali beki huyo wa kimataifa kutoka Togo alitarajiwa kuwasili juzi pamoja na Ngoma lakini ilishindikana kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi na uongozi wa Yanga, hata hivyo.
Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, aliiambia Nipashe jana kuwa wamewasiliana na nyota huyo aliyetoka kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) inayoendelea Gabon na anatarajiwa kuwasili nchini leo kuungana na wachezaji wenzake kupigania kutetea ubingwa wao wa ligi ya Bara.
No comments:
Post a Comment