Guardiola (kushoto)
Kocha Pep Guardiola amemlinganisha Gabriel Jesus na tikiti maji,
baada ya mshambuliaji huyo kinda kuisaidia Manchester City, kupata
ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Westham United, kwenye mchezo wa
ligi kuu ya soka nchini Uingereza, uliopigwa jana
Jesus, 19, alifunga bao lake la kwanza na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji
wa kwanza wa City, kufunga na kutoa pasi ya bao, akicheza kwa mara ya
kwanza dakika zote tisini.
"Huwezi kujua. ni kama tikiti maji. Unatakiwa kulikata na kuona lilivyo". Alisema Guardiola.
Michezo mingine ya jana usiku ya ligi hiyo, ilishuhudiwa Manchester United, ikipata sare ya 9, kwenye ligi ya msimu huu, baada ya kutoka bila ya kufungana na Hull City, kwenye uwanja wao wa Old Trafford.
Hii inamaanisha kwamba hata mchezo unaokuja Man United ikishinda na City ikafungwa United inabaki palepale katika nafasi ya sita.
Nayo Stoke City ikaenda sare ya 1-1 dhidi ya Everton, ambapo katika mchezo huo mshambuliaji wa stoke Peter Crouch alifikisha goli la 100 kwenye EPL
No comments:
Post a Comment