DAR ES SALAAM: Madai mazito! Hivi karibuni taarifa imevuja kuwa msanii
mkali kwenye gemu la Bongo Fleva ambaye kwa sasa anatamba na ngoma
iitwayo Kajiandae kwamba nyumba ‘kali’ anayotamba nayo sasa, amepangiwa
na bilioneaa kijana ambaye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni moja kubwa
jijini.
Habari chengachenga zinaendelea kudai kuwa, mbali na kumpangishia mjengo
mkali huyo wa Bongo Fleva, bilionea huyo kijana ndiye kila kitu kwenye
maisha yake, anamsapoti kwenye muziki na mambo mengine mengi ikiwemo
kumlipia sehemu ya kufanyia mazoezi yaani gym.
Mtoa habari huyo anaendelea kudai, Dimpoz na bilionea huyo wapo karibu
sana kiasi kwamba wanawafanya watu kuwa na wasiwasi nao na kama ingekuwa
ukaribu wao ni wa mwanaume na mwanamke wangehusishwa kutoka kimapenzi!
“Nakwambieni kweli kuna kitu kinaendelea kati ya Ommy na bosi huyo wa
…(anaitaja kampuni), haiwezekani ampangishie nyumba, amlipie gmy na
kumsapoti katika kazi zake za muziki. Lazima kuna kitu kinaendelea kati
yao,” alisema mtoa habari huyo. UWAZI: Sasa wewe unahisi nini
kinaendelea kati yao, si ni washikaji tu?
MTOA HABARI (MH): Hakuna cha ushikaji, ushikaji gani huo, sasa
ngoja nikupe siri, mshikaji wake mkubwa na huyo kigogo ni MwanaFA, sasa
kwa nini hayupo karibu zaidi ya MwanaFA na yupo na Dimpozi? Huwezi
kujiuliza?
UWAZI: Ha Haa haaa! Povu linakutoka sana mzee, kwani hiyo nyumba
aliyopangishiwa Dimpoz wewe unajua ipo wapi na analipiwa shilingi ngapi?
MH: Nyie mfanye uchunguzi, wewe unataka kila kitu nikusafishie picha,
haya ni hivi, nyumba ipo Mbezi Beach, analipiwa shilingi ngapi, anaishi
vipi, kazi kwako na wewe kusafisha picha!
UWAZI: Naona unapaniki mzee, twende taratibu vipi kuhusu hiyo gym
anayolipiwa na huyo kigogo, ipo wapi na analipiwa shilingi ngapi?
MH: Aisee una maswali sana, ninachojua gym inaitwa Colosseum halafu siyo
Ommy Dimpoz tu, mastaa wengi tu wanafanyia mazoezi pale.
UWAZI: Hao pia wanalipiwa na huyo kigogo?
MH: Sijui kaka, mimi nakupa habari hiyo tu kwa leo (akakata simu).
OMMY DIMPOZI HUYU HAPA
Alipotafutwa Dimpoz kwenye anga zake ili aweze kuanika ukweli kuhusu
tuhuma hizo. Dimpoz alipopatikana na kusomewa mashitaka yake ilikuwa
hivi;
DIMPOZ: Sasa ndugu yangu hivi ni kila mtu huwa anatafutwa na kuulizwa
anapoishi, anaishi vipi, nani anamlipia pango au ni mimi tu?
UWAZI: Aaaa! Watu wanaulizwa hasa mastaa, we eleza ukweli tu mzee.
DIMPOZ: Umesema hiyo nyumba ninayodaiwa kupangiwa ipo wapi?
UWAZI: Eti inasemekana ni Mbezi Beach kaka.
DIMPOZ: Dah! Unaona sasa, mimi naishi kwangu Kigamboni kwa hiyo hayo madai hayana ukweli.
UWAZI: Na unahisi ni kwa nini huo ukaribu wako na huyo kigogo unatiliwa
mashaka na watu, na ni kweli kuwa kakulipia gym na anakusapoti kwenye
shughuli zako zingine za kimuziki.
DIMPOZI: Kaka naingia benki, siwezi kuzungumza lingine lolote. Dimpozi alikata simu.
No comments:
Post a Comment