Tuesday, February 7, 2017

Idriss ashindwa kuvumilia na kuyaandika haya, imeanzia kwa sauti ya Wema Sepetu







Mchekeshaji/Mtangazaji na Mshindi wa Big brother Africa Idriss Sultan ameonyesha kutofurahishwa na sauti iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa inasikika sauti ya Wema Sepetu akitoa malalamiko yake na kuzungumzia ishu ya kukamatwa kwake na Polisi.

Inaonekana sauti hizo zimerekodiwa bila Wema Sepetu kufahamu kama anarekodiwa hivyo akajiachia akijua anaongea maongezi ya faragha na waliokwenda kumtembelea.

“Na muendelee kupiga kelele kutembelea watu central na kuwarekodi bila wao kujua kwakua tunachukulia maisha ya watu kama mfumo wa likes na following bila kujua tunawaumiza kiasi gani kwa tunachokifanya’
“Basi tuendelee na tutaona kama tunaowapenda kama tunavyosema tutakua tumewatendea haki, kwa hili nimeshindwa kunyamaza, mnajidai Marafiki na watu wa kweli  kumbe unafki unatujaa’
“Tutaua Familia zetu na kuwa wa kwanza kulia kwenye msiba, UBINADAMU UKWAPI ?  Kama hamjaenda kutoa moral support basi kaeni majumbani kwenu na mposti posti vimachozi 
na unafki wenu sio kutuchafulia hata pale pasafi padogo palipobaki ”

No comments:

Post a Comment