Kikosi cha Jose Mourinho kimeonekana kuongeza wimbi la ushindi baada ya
kuipiga Watford goli 2 kwa 0.Japokuwa United walishinda mchezo huo
hawakufanikiwa kuondoka katika nafasi yao ya 6 baada ya Liverpool nao
kushinda na kuwarudisha katika nafasi yao hiyo.
Ushindi wa Manchester United umewafanya waweke rekodi moja mpya katika
ligi ya Uingereza.United wamekuwa timu ya kwanza kukusanya pointi 2000
katika ligi hiyo.Pointi ambazo ni nyingi zaidi kuwahi kufikiwa toka
kuanzishwa kwa mashindano hayo.
United katika msimamo wa ligi kuu Uingereza safari hii wamepitwa na
Chelsea pointi 11.Lakini United wameipita Chelsea pointi 244 kwa ujumla
wa pointi toka ligi hiyo ianzishwe.Alama hizo wamezipata baada ya
kushinda jumla ya michezo 599 na kwenda sare michezo 203 waliyocheza
kuanzia mwaka 1992.
Si hivyo tu bali United pia ndio timu pekee ambayo ina wastani wa pointi
2 katika kila mechi.Huku Arsenal wakiwakaribia United kwa kuwa na
wastani wa 1.89 na Manchester City wakiwa na wastani wa 1.51.
No comments:
Post a Comment