Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Mwanza jana jioni na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.
Makamu wa Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo leo mkoani Simiyu.
Katika ziara hiyo inayoanza leo tarehe 19/2/2018 na kumalizika tarehe 22/2/2018, Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Kiloleli na kuweka jiwe la msingi na baada ya hapo atazungumza na wanachi Lamadi.
Pia Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa mkoa katika eneo la Nyaumata.
Miradi mingine ambayo Makamu wa Rais ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa Barabara za Lami Bariadi mjini chini ya Programu ya uimarishaji wa Serikali za Mitaa za Mjini.
Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Mwanjoro na kusalimia wananchi siku ya tarehe 20, pia atasalimia wananchi wa Mwanhuzi Mjini, Mwandoya (Meatu)
Tarehe 21, Makamu wa Rais atafungua Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda Tanzania kisha atafungua jengo la Utawala la halmashauri ya Itilima na kusalimia wananchi, kufungua jengo la upasuaji la Samia Suluhu Hassan katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa na kuzungumza na wananchi katika viwanja vya nguzo nane.
Siku ya tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria.
No comments:
Post a Comment