Friday, August 25, 2017

MAREKANI:MFUNGWA AUAWA KWA KUTUMIA SUMU MPYA

Mark Asay alikiri kumuua McDowell, lakini akakanusha kutekeleza mauaji hayo mengine.

Mzungu mtetea ubabe wa wazungu ambaye akliwaua watu kwa sababu ya asili yao miaka 30 iliyopita ameuawa kwa kudungwa sindano yenye sumu.

Mark Asay ndiye mzungu wa kwanza katika historia ya jimbo la Florida kuuawa kwa sababu ya kumuua mtu mweusi, kwa mujibu wa shirika linalofuatilia utekelezaji wa hukumu ya kifo.

Asay, 53, alipatikana na hatia ya mauaji ya watu wawili mwaka 1987 katika eneo la Jacksonville.

Aliuawa saa 22:22 GMT (saa saba na dakika 22 Afrika Mashariki).

Ilikuwa mara ya kwanza kwa sindano yenye sumu mpya kutumiwa kumuua mfungwa.

Jopo la mahakama liliamua Asay aliwaua waathiriwa wake - Robert Lee Booker, mtu mweusi, na Robert McDowell, 26, mzungu wa asili ya Kilatino - kwa kuwapiga risasi usiku ambao alikuwa ametoa matamshi ya ubaguzi wa rangi.

Waendesha mashtaka walisema Asay alikuwa amemchukua McDowell, aliyekuwa amevalia kama mwanamke, akashiriki naye ngono, lakini akampiga risasi baada ya kugundua jinsia yake halisi.

Tangu kurejeshwa kwa hukumu ya kifo mwaka 1976, watu weusi 20 wameuawa kwa makosa ya kuwaua wazungu.

Asay aliuawa kwa kudungwa sindano yenye sumu aina ya etomidate ambayo haijawahi kutumiwa awali Marekani.

Sumu hiyo sasa itaanza kutumiwa badala ya sumu aina ya midazolam ambayo imeacha kutumiwa kwa sababu ya kuwasababishia dhiki watu waliohukumiwa kuuawa wakati wanapouawa.

Etomidate ilichanganywa na sumu nyingine mbili - rocuronium bromide na potassium acetate - kabla ya Asay kudungwa.

Katika mahojiano na kituo kimohc acha habari, Asay alikuwa amesema kwamba hataki kuishi jela maisha yake yote.

Mfungwa huyo alikuwa na chale zenye kuonyesha ubabe wa wazungu. Alikiri kumuua McDowell, lakini akakanusha kutekeleza mauaji hayo mengine.

Alikuwa mungwa wa kwanza kuuawa Florida katika kipindi cha miaka 18.

No comments:

Post a Comment