Ili kufanikiwa lazima kufanya juhudi na kujituma. Hii imemtokea James Msuva baada ya kufanya majaribio na kufuzu kuichezea Mbao FC.
James ni mdogo wake winga wa Yanga, Simon Msuva ambaye sasa ni kati ya wachezaji nyota nchini kutokana na juhudi zake.
James aliyewahi kuzichezea Simba na Yanga U20 na msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara alikuwa akiichezea JKT Ruvu, alitua kwenye majaribio hayo wiki iliyopita kabla ya kupewa majibu hayo ya kufuzu.
Mbao hivi sasa ipo kwenye mikakati ya kukisuka upya kikosi chake kilichoondokewa na karibu nusu ya wachezaji mahiri waliotua Simba, Yanga, Azam FC na kwingineko.
Akizungumza na Championi Jumatano, James alisema anafurahi kuwa mmoja wa wachezaji watakaoichezea Mbao msimu ujao wa ligi kuu.
Alisema baada ya kupata majibu hayo, hivi sasa anasubiria kusaini mkataba atakaopewa wakati wowote kuanzia hivi sasa baada ya kufikia makubaliano mazuri.
“Ninafurahi kuwemo kati ya wachezaji watakaounda kikosi cha Mbao, hiyo ni baada ya kufuzu majaribio haya ya wiki, hivyo muda wowote ninatarajiwa kusaini mkataba,” alisema James anayemudu kucheza namba 7, 9, 10 na 11.
Kwa upande wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mrundi, Etienne Ndayiragije, alithibitisha kufuzu kwa James: “Nina wachezaji wengi waliojitokeza kwenye majaribio ya timu yangu na James ni miongoni mwa wachezaji hao ambaye yeye amefuzu.”
Katika majaribio hayo tofauti na James alikuwepo Amos Abel, aliyewahi kuichezea timu ya vijana ya Yanga na kipa Kabali Faraji, aliyewahi kuzichezea Simba na African Sports iliyoshuka daraja.

No comments:
Post a Comment