Wednesday, June 28, 2017

MAKABILA YENYE MWINGILIANO YAANDALIWA UTARATIBU WA KUPEWA VITAMBULISHO NA SERIKALI

Serikali imesema iko katika hatua za mwisho kukamilisha utaratibu wa kutoa vitambulisho vya utaifa utakaoondoa usumbufu kwa makabila yenye mwingiliano na makabila mengine yaliyopo nje ya Tanzania.

Akijibu swali la nyongeza, Mbunge wa Bunda (CCM) Boniface Getere bungeni leo, (Jumatano) Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba amesema utaratibu wa kutoa vitambulisho unafanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

"Serikali kupitia NIDA ipo katika hatua za mwisho kuwapatia Watanzania vitambulisho vya utaifa, baada ya kupata vitambulisho kutakuwa hakuna usumbufu kwa makabila yenye mwingiliano,"amesema.

Getere amehoji ni lini usumbufu wanaoupata watu wa kabila la wajaluo katika jimbo lake wakati wa usajili wa vyeti vya kuzaliwa utaisha.

Amesema watu hao wamekuwa wakipata matatizo kutokana na kabila lao kuingiliana na wajaluo wa nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment