Thursday, May 11, 2017

UGONJWA WASABAISHA MTOTO KUWA KAMA JIWE!


MTOTO wa umri wa miaka minane (8), Mehendi Hassan, raia wa Bangladesh, amelazimika kutumia muda mwingi akiwa ndani nyumbani kwao, kutokana na kukabiliwa na ugonjwa usiojulikana ambao unafanya sehemu kubwa ya mwili wake kugeuka na kuwa kama jiwe.
Ugonjwa huo unamsababishia maumivu makali mwilini na kumfanya akose marafiki wa kucheza naye, kwa kuwa watoto wenzake wanamuogopa kwa muonekano alio nao.
Wakati usoni anaonekana kutokuathirika sana, Mehendi hawezi kutembea wala kukamata kitu mikononi.
Akiongeza kwa uchungu, mama yake mzazi ameomba serikali ya nchi hiyo kumsaidia mwanawe aweze kuchunguzwa na ikiwezekana apatiwe matibabu ili aondokane na ugonjwa huo wa ajabu na kuweza kuishi kwa furaha kama watoto wenzake.
“Naumia sana ninapoona mtoto wangu anavyosemwa vibaya na wenzake na hata watu wazima kutokana na ugonjwa huo. Wanamuona kama laana,” anasema mama huyo kwa uchungu.

No comments:

Post a Comment