Wednesday, April 12, 2017

Joseph Omog: Sikuamini Kama Tutawafunga Mbao

Kocha wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon akiwa na wachezaji wake mazoezini.
KOCHA wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon, ameweka wazi kwamba kitendo cha wachezaji
wake kushinda mechi dhidi ya Mbao kilim-shangaza hata yeye ku-tokana na kuamini mechi hiyo ingeisha kwa sare au kupoteza.

Omog kwa mara ya kwanza aliweka rekodi ya Simba kupata ushindi ka-tika Uwanja wa Kirumba baada ya kupita miaka saba mfululizo bila ya kuondoka na ushindi.

Kocha huyo ameliam-bia Championi Jumatano kuwa, mechi hiyo ni mion-goni mwa mechi ngumu ambazo amewahi kuku-tana nazo akifundisha soka kwani huwa ngumu kwa timu ambayo im-efungwa mabao mawili kuweza kupindua ma-tokeo.

“Sikuwa na imani kubwa ya kushinda baada ya kufungwa yale mabao mawili japo nilitambua tuna nafasi ya kushinda kwa sababu sisi tuna uzoefu zaidi ya wapin-zani wetu ambao walikuja kuchoka katika dakika za mwisho na sisi ndiyo tuka pata mabao yetu.

“Ila niwapongeze Mbao kwa ushindani ambao wametuonyesha na niseme hii ni moja ya mechi ngumu ambazo nimeku-tana nazo kwenye maisha yangu ya soka kwani kutoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda siyo jambo dogo hata kidogo.

“Sasa tumekaa kwenye uongozi wa ligi na niseme kwamba hiki tuli-chokifanya mbele ya Mbao ndiyo tutakifanya kwe-nye mechi nyingine zijazo ikiwemo mchezo wetu dhidi ya Toto,” alisema Omog.

No comments:

Post a Comment