Sophia Simba
FAGIA fagia ya CCM iliyofanywa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)
imetajwa kwamba itaimarisha chama hicho wala hakitatetereka kwa
kuondolewa vigogo hao.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu ulikuwa ukifanyika jana katika Ukumbi wa
Kikwete mjini hapa kwa nafasi tofauti walisema chama kitakuwa imara.
Wajumbe hao walisema mabadiliko katika chama ni mazuri kutokana na
kukiimarisha chama ambacho kimekuwa na utamaduni wa kufanya mageuzi mara
kwa mara.
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe alisema mabadiliko katika chama
yaliyotimua baadhi ya wanachama ni mazuri kwani yanalenga kukiimarisha
chama.
“Mageuzi katika chama yamefuata hatua zote muhimu na yamefanyika baada ya mwaka mmoja kufanyika uchaguzi,” alisema Bashe.
Alisema kabla ya mageuzi na mabadiliko hayo ya kupunguza wanachama, NEC
ilikuwa na wajumbe wengi 388 ilikuwa kama soko wala si mkutano, lakini
sasa kupungua hadi wajumbe 163, utakuwa mkutano mzuri.
Bashe pia alisema kupungua kwa wajumbe wa Kamati Kuu kutoka wajumbe
kutoka 34 hadi 24, kutaongeza ufanisi ndani ya mkutano huo ambao ni wa
juu katika chama.
Kwa mujibu wa Bashe, idadi kubwa ya wajumbe inaleta migongano ya
kimaslahi badala ya kujadili na kufikia uamuzi katika mikutano ya chama.
Mjumbe wa Mkutano kutoka Iringa, Blastus Mgimwa alisema pamoja na Iringa
kupata pigo la kuondolewa kwa Mwenyekiti wa Mkoa, Jesca Msambatavangu
aliyefukuzwa kwa kukosa maadili, wataenda kujipanga na kuhakikisha chama
kinasimama imara.
Alipongeza mageuzi yaliyofanywa na chama kwa madai kwamba yamekuja kwa
wakati wakati chama kinajiandaa kufanya uchaguzi wa ndani tangu Machi
mwishoni hadi Desemba mwanzoni.
“Mageuzi yamekuja kwa wakati wake, hasa kutokana na msimamo wa
mwenyekiti, Rais John Magufuli kusimamia kwamba wachague viongozi ambao
hawatumii rushwa,” alisema.
Mjumbe mwingine, Mzee Hamad Nassoro alipongeza juhudi za kupunguza idadi
ya wajumbe kutoka katika ngazi ya shina hadi taifa, akasema ilikuwa
gharama kuendesha chama.
“Tunapongeza mpango wa kupunguza idadi ya wajumbe wa mikutano, kwani ilikuwa gharama kubwa kuendesha mikutano hiyo,” alisema.
Kuhusu wanachama 22 waliopewa adhabu mbalimbali ikiwamo ya kuondolewa
wanachama 12 na wengine kupewa onyo kali, alisema ni vizuri kuanza
mwanzoni na watu safi badala ya kubaki na makapi katika chama.
“Ni vizuri kuwa na timu ya watu safi, badala ya kuanza na watu wasio
wasafi katika kutekeleza mageuzi ndani ya chama,” alisema Nassoro.
Mwanachama mwingine, Carolyne Castro na Pascal Manyanda kwa nyakati
tofauti walisema kitendo cha chama kuwa cha wanachama na kuanzia
kuimarisha katika ngazi kutaimarisha chama na kujihakikishia ushindi
katika uchaguzi.
Mjumbe Yusufu Sanga kutoka Makete, alisema amefurahia mageuzi na akasema
kuhusu wanachama waliondolewa kwenye chama ili ifanyike ili kuanza na
wanachama walio safi na wanaokitumikia kwa uaminifu.
Sanga alisema kitendo pia cha kupunguza wajumbe kinaleta ufanisi katika chama na kuongeza imara katika chama.
No comments:
Post a Comment