Thursday, March 9, 2017

BOSI WA SAMSUNG KIZIMBANI KWA KUMUHONGA RASIS BN. 72/-


MTENDAJI MKUU wa kampuni ya kimataifa ya vifaa vya kielektroniki na umeme ya Samsung, Lee Jae-Yong, amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya fedha za ofisi.

Katika kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa nchini Korea ya Kusini, ikitarajiwa kuchukua miezi kadhaa.

Tuhuma zake zinaoainishwa na dhamira ya kukuza baadhi ya maslahi ya kisiasa nchini humo.

Hata hivyo, alivyosomewa mashitaka jana, mtuhumiwa hakuwapo mahakamani na aliwakilishwa na wanasheria wake waliyokana mashitaka yote yaliyosomwa.

Kimsingi, kesi hiyo inaoainishwa na kushirikiana na Rais wa Korea, Park Geun-hye, ikidaiwa alisaidiwa kisiasa na bosi huyo wa Samsung,
Kwa kutumia nafasi aliyo nayo katika kampuni kujinufaisha.

Lee ni Makamu Mwenyekiti wa Samsung, pia anakaimu nafasi ya ubosi mkuu, kutokana aliyekuwa kwenye nafasi hiyo kabla –baba yake aitwaye, Lee Kun-hee,kuugua tangu mwaka 2014.

Katika tuhuma hizo, Lee anadaiwa pamoja na mabosi wengine wanne, waligawa fedha Dola za Marekani milioni 36 (Sh. bilioni 79.2)
kwa rafiki wa karibu wa rais aliyeko matatani, lengo lilikuwa kufanikisha maslahi ya kisiasa, ambayo ni kinyume na sheria za nchi.

Waendesha mashitaka walidai kuwa, hilo lilifanywa ili kuleta mabadiliko ya kampuni wakipata kuungwa mkono na serikali iliyokuwa madarakani.

Mnamo katika kikao cha bunge mwezi Desemba iliyopita, Lee alikiri kutoa fedha hizo, ingawa anapinga vikali dai la kuwapo dhamira mbaya kwa namna yoyote ile.

Lee katika maelezo yake, anasema sasa anajutia anachokitaja kuwa wema aliyoufanya ambao sasa unamgharimu.

Wakati akitarajiwa kwa kiasi kuhalalishwa katika nafasi aliyo nayo ya ubosi mkuu wa Samsung, wapo wanaomponda kwamba hata nafasi hiyo anayoishikilia sasa, inatokana na bahati ya kuzaliwa ndani ya ukoo unaomiliki kampuni na si umahiri wa kazi.

Sakata linalomkabili lilianza tangu Oktoba mwaka jana, pale kelele za kisiasa zilianza kusikika rasmi bungeni na baadaye, akaitwa rasmi kuhojiwa na sasa liko katika mustakabali wa kisheria kutafutiwa maammuzi, kupitia shitaka hilo la jinai.

L Makala hii imeandaliwa kwa mujibu wa taarifa za mtandao

No comments:

Post a Comment