Friday, March 31, 2017

AZAM NA NDANDA KUZICHAPA APRILI 5


Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetangaza mchezo wa hatua ya robo fainali ya tatu ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara, utachezwa Aprili 5 kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa kuanzia majira ya saa 1:00 usiku.

Aidha, mchezo wa robo fainali ya mwisho baina ya Yanga dhidi ya Tanzania Prisons utafanyika Aprili 22 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Washindi wa michezo hiyo wataungana na klabu za Simba na Mbao FC kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Simba ilitinga hatua hiyo baada ya kuitupa nje Madini FC ya Arusha kwa kuifunga bao 1-0 huku Mbao FC ikitinga hatua hiyo baada ya kuitupa nje Kagera Sugar kutokana na ushindi wa bao 2-1.

No comments:

Post a Comment