Ametoa
kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Februari 15, 2017) wakati akizungumza
na maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa
michezo wa mjini Kibaya, wilayani Kiteto, mkoani Manyara.
Waziri
Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita
mkoani Manyara, alisema: “Hatutakubaliana na wachochezi. Hatutakubaliana
na yeyote atakayesababisha kifo. Tukibaini kuna uchochezi, tutawasaka
wahusika na kuwashughulikia,” alisema.
“Hapa
kulikuwa na majina ya ajabuajabu, hatutakubali Kiteto iitwe Soweto au
Kossovo, hapa ni Tanzania. Hatuwezi kuishi kwa kubaguana, ni lazima
tuheshimu maamuzi ya wazee wetu wa kimila ambao wamesimamia zoezi hili
ili kurejesha amani ya Kiteto,” alisema.
Alisema
zamani Kiteto kulikuwa hakuna lugha ya amani lakini hali kwa sasa
imebadilika na kuwa nzuri na akasisitiza kwamba hakuna kurudi nyuma.
Alisema
anamshukuru Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda kuwa kufuatilia
suala hilo na kuunda tume ya kutafuta amani wilayani Kiteto.
“Nilipoingia madarakani, nami nilianza kufuatilia suala hilo ili nijue
chanzo hasa ni nini. Nikabaini kuwa mgogoro mzima umechangiwa na
chokochoko tu za watu wachache,” alisema.
Mapema,
viongozi wa kimila walimkabidhi Waziri Mkuu rungu, jembe dogo na jani
la mti wa asili (Kimasai unaitwa elisibie) ikiwa ni ishara amani ya
kukomesha mapigano baina ya wafugaji na wakulima. Pia alishiriki dua ya
kuombea amani ambayo iliongozwa na viongozi wa dini.
No comments:
Post a Comment