Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers
Sianga amesema watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha mkoani Mwanza
kwa sababu ya kukosa dawa za kulevya mtaani kama walivyozoea.
Kamishna
Sianga amesema taarifa hiyo ameipata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
hali inayomaanisha mafanikio ya mapambano ya dawa hizo, ambapo kwa sasa
usambaaji wake umepungua mtaani kwa kiasi kikubwa.
"Nimeongea
na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ameniambia kwamba kuna watu wwili wamefariki
sababu walikuwa drug addict na sasa dawa hizo hazipo mtaani" Amesema
Sianga.
Sianga
amesema mara baada ya kupokea kijiti cha mapambano kutoka kwa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mamlaka hiyo imeendelea na moto huo
huo, na kwamba kwa hivi sasa timu yake hailali, ikiendelea na mapambano
kila siku na kwamba hata jana, kuna mtuhumiwa mkubwa wa dawa za kulevya amekamatwa.
"Leo (jana) asubuhi tumemkamata mtuhumiwa mmoja mkubwa wa dawa kulevya, tupo naye tunaendelea kumuhoji, mengi yataibuka" alisema Kamishna Sianga
Kuhusu
kuendelea kutumia mbinu iliyokuwa ikitumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam paul Makonda ya kutaja majina hadharani,, Kamishna Sianga alisema
hatatumia njia hiyo kwa kuwa kutaja majina ya watu hadharani kunaweza
kuiingiza serikali katika matatizo maana kuna watu wengine wanaweza
kutoa majina ya watu kwa sababu ya chuki binafsi.
Amesema njia anayoitumia ni kuwakamata na kuwahoji kimyakimnya na wakishajiridhisha hatua nyingine za kisheria zinafuata.
Katika
hatua nyingine, Sianga amesema Tanzania iko makini katika
kuwashughulikia wahusika wakubwa wa dawa za kulevya duaniani tangu miaka
mingi iliyopita, akitolea mfano mtuhumiwa mmoja wa kike ambaye ni gwiji
katika biashara hiyo au 'King Pin', ambaye hivi sasa amefungwa katika
magereza ya Tanzania tangu mwaka 2010
"Tulimkamata
mmoja kati ya watu waliokuwa wametajwa kama king pin wa dawa hizo
nchini Marekani, alikuwa ameshindikana, na huko Marekani alikuwa na kesi
zaidi ya 40, lakini alikamatwa hapa na amefungwa tangu mwaka 2010, yuko
gerezani nafikiri kama siyo Keko, ni Segerea". Amesema Sianga.
No comments:
Post a Comment