Thursday, February 2, 2017

TAARIFA YA JWTZ KUHUSU MAUAJI YA KONDAKTA MKOANI TANGA

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4438 la tarehe 28 Januari 2017, Habari leo   la tarehe 29 Januari 2017 na baadhi ya vyombo vya habari vikihusisha mauaji ya kondakta wa daladala na Wanajeshi Mkoani Tanga.



Tunapenda  kuwataarifu wananchi kwamba kwa mujibu wa jeshi la polisi watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi hilo ni wanne (4),mmoja kati yao ni Mwanajeshi ambaye ni mzazi wa msichana anayetuhumiwa kusababisha tukio hilo.



Hivyo Mwanajeshi huyo anashikiliwa kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi katika uchunguzi kwa kuwa tukio hilo lilifanyika nyumbani kwake. 



Hakuna Wanajeshi waliohusika katika tukio hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, kambi za Jeshi wanaishi Wanajeshi pamoja na familia zao hivyo kuhusisha moja kwa moja mauaji hayo na Wanajeshi  mkoani Tanga ni kuupotosha umma.



Wito unatolewa kwa vyombo vya habari kuripoti habari zenye ukweli.Habari zisizo za kweli zinapotosha umma na kujenga taswira potofu kwa wananchi dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. 



Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

S.L.P  9203,   

Dar es Salaam,  

Tanzania.

No comments:

Post a Comment