VITA ya kupambana na dawa za kulevya ikiwa imeshika kasi nchini na
kusababisha kupungua kwa mihadarati sokoni baada ya wafanyabiashara hiyo
kuhofia kukamatwa, watumiaji 'mateja' wameibuka na vilevi mbadala.
Uchunguzi wa Nipashe umegundua kuwa 'mateja' ambao bado wapo mitaani
baada ya watumiaji wengi kuonekana kukimbilia katika nyumba za matibabu,
wamelazimika kutumia vileo mbadala ili kukidhi haja ya miili yao.
Uchunguzi katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam ambayo huwapo watumiaji
wengi wa dawa za kulevya, umebaini kuwa 'mateja' wamehamia kwenye vileo
kama mafuta ya petrol, ugoro na gundi ya viatu baada ya kukosa dawa za
kulevya.
Vita dhidi ya dawa za kulevya nchini ambayo imepata msukumo mpya tangu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ataje watu 65 waliotakiwa
kuisaidia polisi kuhusu biashara ya mihadarati wiki mbili zilizopita,
ilipata nguvu zaidi wiki iliyopita kutoka kwa IGP, Ernest Mangu.
No comments:
Post a Comment