Showing posts with label AFYA. Show all posts
Showing posts with label AFYA. Show all posts

Friday, September 29, 2017

FAIDA 10 ZA KUTUMIA PILIPILI KATIKA MLO WAKO


 Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu:
Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari.
 Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.

Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili

Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi!

Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer)

Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.

Kula pilipili usaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.

Saturday, September 16, 2017

WIZARA YA AFYA YAPIGA MARUFUKU KUVUTA SIGARA HADHARANI

Wizara ya Afya Zanzibar imepiga marufuku uvutaji sigara kwenye mikusanyiko ya watu ili kuwanusuru watu wasiovuta kuathirika na moshi.


Mkurugenzi Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Jamala Adam Taib, akifungua warsha ya kuimarisha kanuni za kupambana na matumizi ya tumbaku visiwani Zanzibar, alisema uvutaji sigara ni chanzo kikubwa cha ongezeko la maradhi yasiyoambukiza ikiwamo saratani, kisukari, mapafu na homa ya ini.

Alisema licha ya kuwa Zanzibar haizalishi tumbaku na haina viwanda vinavyosarifu bidhaa hiyo, wananchi wanaathirika kwa moshi wa sigara.

Alisema utafiti unaonyesha asilimia kubwa ya watu wanaofariki kutokana na maradhi hayo, chanzo chake ni uvutaji sigara.
Aidha, alisema asilimia 15 ya vifo hivyo vinawafika watu wanaovuta moshi wa sigara zinazovutwa na watu wengine.

“Ili kufanikisha lengo  hili nazishauri taasisi za serikali, jumuiya za kiraia na jamii kwa jumla kuunga mkono kanuni inayokataza sigara kuvutwa kwenye mikusanyiko ya watu na kanuni nyingine zinazoundwa ili kulinda afya za wananchi,” alisema.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Ghirmay Andemichael, alisema zaidi ya watu milioni saba, wanapoteza maisha kila mwaka duniani kutokana na matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku.

Alisema kama hatua hazitachukuliwa za kuandaa mikakati ya kupunguza matumizi ya bidhaa za tumbaku, nusu ya watumiaji wa bidhaa hizo watafariki kwa kuwa tumbaku ni hatari kwa kila mtu na inatabia ya kuua kimya kimya.

Aliishauri serikali, jamii na washirika wa maendeleo kufanya juhudi za ziada kuhakikisha kanuni zinazokataza matumizi ya tumbaku Zanzibar zinaimarishwa na zinatekelezwa kikamilifu.

Aliahidi kuwa WHO itandelea kutoa kila msaada katika kuimarisha kanuni hizo ili kuiwezesha Serikali ya Zanzibar kufikia lengo la maendeleo endelevu la kupunguza vifo vinavyotokana na maradhi yasiyoambukiza kwa asilimia 3.4, ifikapo mwaka 2030.

Akizungumzia Azimio la WHO na mikakati ya kimataifa katika mapambano ya matumizi ya tumbaku, Dk. William Maina, alisema nchi zinapaswa kuongeza kodi ya bidhaa za tumbaku kwa lengo la kuzipandisha bei ili baadhi ya watu washindwe kuzitumia.

Alizitaja njia nyingine kuwa ni kupunguza matangazo ya bidhaa hizo katika vyombo vya habari, kuweka ilani ya madhara ya tumbaku katika vifungashio vya sigara na nchi jirani kushirikiana katika mapambano ya matumizi ya tumbaku.

Sunday, August 13, 2017

KUBEMENDA MTOTO

Kumbemenda mtoto ni mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwenzi wake hasa kipindi mtoto bado ni mchanga na ananyonyeshwa.


Hii ni dhana iliyopo katika jamii mbalimbali, na inadhaniwa hutokea kwa sababu mtoto kunyonya maziwa yenye mbegu za kiume zilizoingia kwenye maziwa baada ya kufanya mapenzi.

Je, kuna ukweli wowote?
Hapana. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa!
kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa. dhana ya kuwa shahawa huingia kwenye maziwa na kumuathiri mtoto sio sahihi.

Ni baada ya muda gani mwanamke aliyejifungua anaweza kufanya mapenzi?
unaweza kuanza kufanya mapenzi tena baada ya maji maji yenye damu ya uke (lochia) kuacha kutoka ambayo ni kama wiki 3 mpaka 4 baada ya kujifungua, na wewe kujisikia vizuri na kuwa tayari kushiriki katika mapenzi. pia, mnaweza kusubiri mpaka wiki 6 zipite toka ulivyojifungua.

Je, kuna athari yoyote ya kufanya mapenzi baada ya kujifungua?
Kufanya mapenzi baada ya kujifungua hakuwezi kuleta madhara kwa mtoto endapo hamna maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu). ikiwa mwanaume ana vvu anaweza kumuambukiza mama na kisha mtoto kuambukizwa kupitia maziwa ya mama.

Ikiwa mnafanya mapenzi kabla ya damu damu ya ukeni kukata, maambukizi ya bakteria yanaweza kutokea kwenye tumbo la uzazi (endometritis). pia kuna uwezekano wa mama kupata ujauzito miezi 6 ya kwanza ya kunyonyesha.

Nini kinasababisha afya ya mtoto kuzorota?
Kama tulivyoona, kufanya mapenzi hakusababishi mtoto kubemendwa. afya ya mtoto inaweza kuzorota kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo;
  • Kukosa maziwa ya mama ya kutosha
  • Mtoto kushindwa kunyonya vizuri
  • Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na viritubisho vya kutosha.
  • Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.
  • Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.
  • Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).

Kufanya mapenzi na mwenzi wako hakusababishi mtoto kubemendwa. baada ya kujifungua mtoto hutegemea kupata lishe bora kutoka kwenye maziwa ya mama, hivyo nyonyesha mtoto wako vizuri. ukiona ukuaji wake unazorota, onana na daktari.

Monday, June 19, 2017

MAJI NI TIBA SOMA HII


Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza tiba kwa kutumia maji:
Ifuatayo ni kanuni ya jumla ya namna ya kuyatumia maji ya kunywa katika kujikinga na kujitibu na maradhi au magonjwa mbalimbali mwilini. Kwa sababu ili maji yawe ni dawa basi kuna kanuni ya kuyanywa maji hayo.

Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya maji ni; kunywa nusu ya uzito wako katika aunsi (ounces) ugawe mara mfululizo utakaoufuata kwa siku nzima. Kiasi kidogo chini au juu ya hiki, kinakubalika. Aunsi 1 = miligramu 31.25.

Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya chumvi ni, Robo tatu gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji, nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji.

Pengine umeshageuza kichwa na kujisemea, “Wewe ni kichaa…..hicho ni kiasi kingi sana cha maji”.

Ukweli ni kuwa, ni rahisi kunywa hivyo hasa tukitumia sentensi, glasi 8 za maji zikigawanywa mara nane kwa siku (glasi 1 = ml 250 au robo lita).
Mfano, kwa mtu mwenye uzito wa kilogramu 75:


  • Badili kilogramu kwenda aunsi kwa kuzidisha mara 2.2. Hivyo, 75×2.2 = aunsi 165.
  • Tafuta nusu ya aunsi kwa kugawa aunsi na 2. Hivyo, aunsi 165/2 = aunsi 82.5.
  • Gawanya mara mfululizo utakaoamua kuufuata kwa siku nzima, mfano mara 8 kwa siku. Kwa hiyo aunsi 82.5/8 = aunsi 10.3.
  • Badili aunsi kuwa miligramu za maji. Aunsi 1 = miligramu 31.25. Kwa hiyo aunsi 10.3×31.25 = miligramu 322.

Kwa hiyo itampasa mtu huyo mwenye uzito kilo 75, kunywa ml 322 za maji mara nane kwa siku.

Namna anavyopaswa kufuata hiyo ratiba mara 8 kwa siku:
1) Akiamka tu (mfano saa 12 kamili asubuhi), cha kwanza atakunywa maji ml 322. ataendelea na shughuli zake za asubuhi

2) Nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi (yaani saa 12:30 asubuhi), atakunywa maji ml 322. atasubiri nusu saa ipite ndipo atapata chakula chake cha asubuhi (itakuwa saa 1 kamili asubuhi).

3) Kisha kula chakula cha asubuhi, atahesabu masaa 2 na nusu ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 3 na nusu asubuhi).

4) Atahesabu masaa 2 tena ndipo atakunywa tena ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha mchana (itakuwa saa 6 mchana) kwa hiyo nusu saa baadaye atakula chakula cha mchana (yaani saa 6 na nusu mchana).

5) Atahesabu yapite masaa 2 na nusu baada ya chakula cha mchana ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 9 kamili alasiri).

6) Atahesabu masaa 2 na nusu yapite ndipo atakunywa maji ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha jioni (itakuwa saa 11 na nusu jioni). Nusu saa baadaye atakula chakula cha jioni (itakuwa saa 12 kamili jioni).

7) Kisha kula chakula cha jioni, atahesabu masaa 2 na nusu tena ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 2 na nusu usiku).

Muda wowote atakapokwenda kulala kuanzia saa 4 usiku atakunywa tena maji ml 322 kumalizia mara 8 zake kwa siku.

Huyo alikuwa na kilo 75, sasa na wewe andika uzito wako na utumie fomula hiyo hapo juu ujuwe ni kiasi gani cha maji unahitaji kwa siku na kisha ufuate mara hizo 8 kama zilivyopendekezwa hapo juu. Kwa staili hii ndipo maji huwa ni zaidi ya dawa.

Kila mmoja wetu sasa anaweza kutumia uzito wake kwa kutumia fomula hii na kujua ni kiasi gani cha maji anahitaji kwa siku.

Kumbuka, Kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ni kiasi cha chini kabisa, lakini mahala pazuri pa kuanzia, ikiwa ni mtu unayejishughurisha zaidi na mazoezi au unaishi katika mazingira ya joto zaidi, utahitaji zaidi ya hapo.

Sasa, hutakubali kuwa kunywa maji kwa protokolo hii ni kazi rahisi?.
Ikiwa haunywi kiasi hiki cha maji kwa sasa, unapaswa kuanza kuongeza kiasi cha ziada kwa taratibu sana. Hii itaupa nafasi mwili kujirekebisha kuendana na kiasi ulichoanza kukiongeza, na ikiwa hautaupa mwili muda wa kujirekebisha, basi maji yatakuwa kama dawa ya kukojosha (diuretic), yakisukuma madini na vitamini za mhimu nje ya mwili, pengine na kukusababishia madhara zaidi kuliko faida.

Watu wazee na watoto wadogo wanatakiwa kuanza kuongeza maji kufikia mahitaji yao kwa taratibu zaidi.

Kwa kutumia mfano wa uzito hapo juu, itakupasa kuanza na glasi 3 siku ya kwanza huku ukiongeza glasi moja zaidi kila siku inayofuata mpaka ufikie glasi zote 8.

Kumbuka kuwa, kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi na kula chumvi robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji, ni kanuni ya kimakisio tu. Baadhi ya wengine watahitaji maji zaidi wakati wengine watahitaji chumvi zaidi. Baada ya muda, mahitaji ya mwili kwa maji na chumvi yanaweza kuongezeka kidogo zaidi sababu ya mazingira ya joto, mazingira ya baridi au mazoezi ya viungo.

Kila mmoja lazima apate kujua kiasi cha mahitaji ya mwili wake kwa maji kuanzia sasa.

Kamwe usinywe zaidi ya aunsi 33.8 (lita moja) za maji kwa wakati mmoja ukiwa umekaa au umesimama.

Watoto wadogo kuanzia miaka 2 mpaka 12, hasa wale wepesi kujishughulisha na mazoezi wanahitaji asilimia 75 mpaka 100 za aunsi za maji katika uzito wao kwa sababu miili yao inakua muda wote na kila seli katika miili yao inayokua inayahitaji maji haya ya ziada (mytosis).

Tiba hii ya maji haitumiki kwa watoto chini ya miaka 2.

Chumvi ya kawaida ya mezani iliyoongezwa madini ya iodini, itakusaidia kidogo, chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini mengine mengi ya ziada zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake. Chumvi ya baharini pia huwa na radha nzuri, nyeupe na umajimaji kidogo.

Namna bora za kula chumvi:
Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.

Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.

Ukiona viwiko, vidole, miguu, mikono au kope za macho zinavimba (kuvimba kusikotokana na ajali au jeraha), au unaharisha zaidi, usitumie chumvi kwa siku 2 mpaka 3, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena, lakini ichukuliwe taratibu. Kamwe usitumie chumvi zaidi ya robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji.

Kumbuka chumvi ikizidi hupelekea kuharisha.
Dr.Batmanghelidj anasema, kunywa maji matupu kunaweza pelekea mwili kupoteza baadhi ya madini na vitamini zake mhimu nje ya mwili na hivyo kutozipa seli muda wa kutosha kuyatumia maji. Inashauriwa kutumia vidonge vyenye vitamini nyingi kwa pamoja (multivitamins) katika kila mlo wako ili kurudishia kile kitakachokuwa kimepotea (hasa ikiwa haufanyi mazoezi na kula kiasi kingi cha mboga za majani).

Uvimbe utakapokuwa umepotea au umeacha kuharisha, unaweza kuendelea na mpango wako wa kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ingawa mara hii utayachukua kwa kiasi kidogo.

Kwa siku nzima, anza kuongeza kiasi cha unywaji wako wa maji mpaka ufikie tena nusu ya uzito wako katika aunsi, anza pia kuchukua chumvi pamoja na maji. Unatakiwa kuhakikisha kuwa unapata gramu 150 za madini ya iodine kwenye “multivitamins” zako kila siku mpaka gramu 450 kwa siku.

Kisha kunywa maji, maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa 2 mpaka 2 na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri.

Ikiwa inakulazimu kukojoa (peeing) chini ya muda wa masaa 2 tangu unywe maji, utalazimika kuacha kunywa maji matupu, jaribu kunywa juisi (uliyotengeneza mwenyewe) ya chungwa, ya limau au ya zabibu au juisi nyingine yeyote isipokuwa kwa watu wanaosumbuliwa na pumu (asthma) ambao hawatakiwi kunywa juisi ya chungwa.

Wakati huo huo mhimu kukumbuka kuongeza robo tatu gramu za chumvi katika kila nusu lita ya juisi yako.

Ikiwa kunywa juisi hakutasaidia kupunguza kwenda bafuni kila mara, jaribu kunywa maji huku ukila mkate. Unaweza kuongeza krimu ya siagi au jamu kwenye mkate wako (the magic bagel).

Kisha kutumia mkate siku moja au mbili unaweza kupunguza sasa kiasi cha mkate mpaka nusu yake, robo yake na mwisho juisi pekee pamoja na mlo wako.

Utapaswa kurudi taratibu tena kutoka kunywa maji juisi mpaka kunywa maji matupu tena, baada ya siku kadhaa itakupasa kujaribu aunsi 2 za maji matupu nusu saa kabla ya chakula, kesho yake aunsi 4, siku inayofuata itakuwa aunsi 6 kisha 8 na kuendelea mpaka ufikie kiasi chako unachotakiwa.

Ikiwa kunywa maji pamoja na kula mkate au katika juisi hakukusaidii kupunguza kwenda bafuni, Glasi ya maji (ml 250) matupu ikiongezwa na kijiko (kijiko cha chakula) kimoja cha asali au sukari halisi au walau sukari nyeupe kutakutatulia tatizo hili ukiongeza na chumvi 1/8 ya kijiko cha chai , tikisa na kisha kunywa mchanganyiko huo.

Bilashaka umewahi kusikia msemo, “Kwa sehemu kubwa tumetokana na maji”, hii ndiyo sababu zaidi ya asilimia 94 ya damu yetu ni maji, zaidi ya asilimia 85 ya ubongo wetu ni maji, huku zaidi ya asilimia 75 ya sisi ni maji.

Muda gani unywe maji fomula ya jumla:
Kitu cha kwanza kufanya mara uamkapo tu, ni kunywa glasi 2 za maji (ml 500) kwakuwa umetumia glasi 2 za maji kwa kulala mpaka asubuhi.

Kunywa glasi 1 robo saa au glasi 2 nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni, kisha hesabu masaa 2 au 2 na nusu kila baada ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni bila kunywa wala kula chochote, ndipo unywe glasi 1 ya maji.

Kunywa glasi 1 ya maji kila uendapo kulala.
Muda wowote uamkapo usiku kwenda bafuni, kunywa nusu glasi ya maji na kipande cha chumvi kisha rudi kulala.

Muda wowote unapopatwa na kiu kunywa maji.
Kwanini unywe maji robo lita, robo saa kabla ya kula, au nusu lita, nusu saa kabla ya kula?:

Wanyama wote hunywa maji halisi (plain water). Ikiwa utawachunguza paka na mbwa, mara zote hunywa maji na kusubiri wastani wa nusu saa kabla ya kula. Ratiba inabadilika wanapokuwa wanatibiwa, hapa hunywa na kisha hula papo hapo ama baadaye.

Mfululizo huu ni mhimu ili kubaki na afya bora.
Unapokunywa maji na kusubiri nusu saa kabla ya kula, maji yanaenda tumboni na kuziamsha tezi kutoa kemikali (homoni) kuzifunika kuta za tumbo ili kuzirinda dhidi ya haidrokloriki asidi ambayo huzarishwa wakati chakula kinawekwa mdomoni.

Maji na kemikali hizo kisha huenda kwenye utumbo mdogo ambako kemikali hizi hukaa kusubiri chakula kitakachokuwa kinakuja baadaye. Maji hayo huru, yanauacha utumbo mdogo na kwenda katika seli zote za mwili na kuzijaza (kuzinyweshea) maji kama vile unavyonywesha bustani. Baada ya seli kuwa zimenyeshewa, maji yanayobaki kisha yanasukumwa tena kwenda tumboni ili kunyeshea chakula kilichofika.

Nguvu zetu hazitokani na vyakula tunavyokula, bali zinatoka katika maji ambayo yanaiweka atomu ya haidrojeni katika chakula.

Tunatembea katika haidrojeni.
Vyakula tulavyo hutupatia vitamini na madini tunayoyahitaji ili kubaki katika afya.

Ikiwa haunywi maji halisi (glasi 1 au 2) kabla ya kula chakula na kusubiri (robo saa au nusu saa), basi mwili lazima ujikope maji wenyewe!.

Kama mwili utakopa maji toka katika damu, basi ateri lazima zipunguze vipenyo vyake na moyo lazima utumie nguvu nyingi ili kusukuma damu ambayo ni nene (nyingi), kitendo hiki tunakiita ‘shinikizo la damu’(BP).

Ikiwa mwili utajikopa maji toka katika ubongo, utapatwa na ‘kichwa kizito’ au kichwa kuuma ambacho kinaweza pelekea maumivu ya kichwa.

Ikiwa unakunywa alikoholi (pombe) na inavuta maji toka kwenye ubongo, utapatwa na kutokujisikia vizuri au uchovu (hangover).

Watu wanaoishi katika nchi za baridi huweka alikoholi kwenye tenki zao za gesi ili kuvuta maji ndani ya gesi na hivyo kuifanya gesi isigande.

Kokote katika ogani au tishu mwili utakakokopa maji, lazima ogani au tishu hiyo iachiwe madhara na hivyo kusababisha maumivu ama ufanyaji kazi wa ogani au tishu hiyo usio wa kawaida kama vile kufunga choo (constipation).

kufunga choo au kupata choo kigumu sana kunatokea wakati mwili umekopa maji toka katika utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana kunakopelekea taka za mwili kusimama kwenye kuta za utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana (colon). Wakati mambo yako yanapokuwa na umajimaji, huteleza yenyewe chini bila kutumia nguvu yoyote.

Kila tunapopumuwa hewa nje (exhale) tunapoteza maji!.
Ikiwa utahema juu ya kioo, utauona ukungu (maji). Tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumuwa tu kila baada ya masaa 24!!.

kama mwili utakopa maji toka mapafuni, utapatwa na pumzi fupi itakayopelekea upatwe na pumu (asthima) na matatizo mengine yanayohusiana na mfumo wa upumuwaji.

Mapafu na Moyo vinauhusiano wa karibu, kwa hiyo kama mwili utakopa baadhi ya maji toka katika mishipa ya moyo, utapatwa na maumivu ya moyo ambayo yanaweza kurahisisha kutokea kwa shambulio la moyo (heart attack).

Mishipa inahitaji damu na maji wakati unafanya mazoezi, kwa hiyo kama unatakiwa kula chakula na kisha kutembea au kupandisha ngazi (za ghorofa) na una upungufu wa maji (dehydrated), unaweza ukapatwa na pumzi fupi, shambulio la pumu, utapatwa na maumivu ya moyo (angina) au kukakamaa kwa mishipa (cramps).

Ndiyo maana wanasema; kamwe usiende kuogelea mara tu baada ya kumaliza kula kwa sababu mishipa itakakamaa.

Mwili unapokuwa katika kazi yake ya umeng’enyaji chakula, huielekeza (diverts) damu toka katika mikono na miguu kwenda katika utumbo mdogo ili kusaidia umeng’enyaji wa chakula.

Baadhi ya vyakula ni rahisi kumeng’enywa na vinawezeshwa na maji pekee, kama vile matunda na mboga za majani.

Vinywaji vingine (liquid beverages) kama vile kahawa, chai, soda na juisi, siyo maji kwa mwili. Hivi ni vyakula pia kwa sababu ulimi unaipata radha ya viongezi (additives) na siyo radha ya maji halisi, na hivyo tumbo litaitowa haidrokloriki asidi. Mwili utakishughurikia kinywaji hicho kama chakula.

Utafaidika na baadhi ya maji kama vile katika matunda na mboga za majani kwa masharti ya kinywaji hicho kutokuwa na kafeina (caffeine).

Kafeina ni kikojoshi (diuretic), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili.
Magonjwa mengine yanayoweza kuepukika kwa kunywa maji kabla ya kula ni pamoja na vidonda vya tumbo, tumbo kunyonga, kiungulia, mafuta yaliyozidi, kansa ya utumbo mdogo, kukinaishwa na chakula, na ernia.

Kunywa maji masaa 2 au 2 na nusu baada ya chakula kunasaidia kumalizia umeng’enyaji wa chakula na kuunywesha mwili maji baada ya kukaukiwa kulikosababishwa na kazi ya umeng’enyaji wa chakula.

kunywa maji ya kawaida katika joto la kawaida.
Magonjwa mengine yanayotibika au kukingika kwa kutumia tiba ya maji ni; Kansa, kisukari, kifua kikuu (TB), shinikizo la damu(BP), mfadhaiko (stress), matatizo ya moyo na kuzimia, magonjwa ya tumbo, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya Ini, pumu (Asthima), mzio (Allergy), chunusi, homa, kupunguwa nguvu na kinga ya mwili, matatizo ya kina mama, magonjwa mengine ni pamoja na homa ya uti wa mgongo, kansa ya kizazi, kikohozi, kuharisha, nyongo, matatizo ya tumbo, kupungua uzito, upungufu wa damu (anaemia), vichomi, vidonda vya tumbo, utipwatipwa, kuzeeka mapema, na magonjwa mengine mengi.

Tiba hii ni nzuri kwa wote, wagonjwa watapona na wazima watabaki na afya bora na kujirinda dhidi ya maradhi kwa maisha yao yote.

Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj: ”Kuna maajabu zaidi ya milioni katika glasi moja ya maji kuliko katika dawa yeyote utakayoandikiwa na daktari au muuguzi wako”. Mwisho wa kunukuu

Angalizo:

  • Ikiwa hauendi chooni walau mara tatu kwa siku,unapaswa kumwona daktari kabla ya kuanza tiba hii.
  • Figo zako lazima ziwe zinafanya kazi vizuri, hii inamaanisha, kiasi cha maji unachokunywa lazima kiwe karibu sawa na unachotoa.
  • Wakati huo huo, kwenda chooni mara nyingi kwa siku kunaweza kukusababishia kupoteza vitamini mhimu, madini na elektrolaiti na kukufanya vibaya zaidi ya vizuri.
  • Unatakiwa kuwa makini sana unapoanza kuongeza uchukuaji wa maji mwilini, anza pole pole kwa kuongeza glasi 1 kila siku mpaka utakapofikia nusu ya uzito wako katika aunsi. lazima uupe mwili muda wa kujirekebisha baada ya kuzoea vinywaji kama kahawa, chai na soda, kwa kuwa vinywaji hivi huufanya mwili kujiendesha kwa namna nyingine.
  • Unaweza kuumwa na kichwa au unaweza usijisikie vizuri tu siku tatu mpaka wiki moja za kuanza tiba, usiache kunywa maji kwakuwa hayo si madhara bali ni dalili kuwa taka za sumu zimeanza kuondoka mwilini, baada ya muda utarudi katika hali yako ya kawaida.
  • Tunashauri watu wenye matatizo ya figo, Ini na moyo, kutofuata tiba hii mpaka watakapopata ruhusa ya daktari na muongozo sahihi.
  • Usinywe maji zaidi ya lita 3.78 kwa siku.
  • Usinywe maji kuanzia lita moja kwa pamoja au ukiwa umekaa katika mkao mmoja iwe kusimama au kukaa.

Kumbuka pia kuwa hii ni elimu tu na siyo kumuondoa daktari wako au chaguo lako la kutumia dawa, ni programu iliyopendekezwa kwa manufaa yako.

Thursday, June 1, 2017

UTAFITI : KANSA YA MATITI VITAMINI D NDIYO KINGA KUBWA


Vitamin D, ambayo kwa kiasi kikubwa hupatikana kwa ngozi kupata mwanga wa jua, ina faida nyingi muhimu za kiafya mwilini na utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa vitamin hiyo ndiyo msingi mkubwa wa kuzuia magonjwa mbalimbali mwilini.

Utafiti huo umebaini kuwa vitamin D ni muhimu kwa sababu kiasia cha asilimia 10 ya vinasaba (genes) vya mwili wa binadamu vinaitegemea vitamin hii kufanya kazi yake, kikiwemo kinasaba kinachohusika na uzuiaji na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na yale ya uvimbe.

Katika utafiti huo ambao pia umeelezewa kwa kina na Dr Mercola wa nchini Marekani katika mtandao wake, imeoneshwa kwamba ukiwa na Vitamin D ya kutosha mwilini, Kolestrol mbaya hushuka na pia huongeza mara mbili uwezo wa mwili kujikinga na saratani ya matiti.

Vilevile utafiti huo umebainisha na kugundua kwamba, kuna uhusiano mkubwa kati ya upungufu wa Vitamin D mwilini na watoto taahira. Ugunduzi huu ni muhimu sana, hasa kwa akina mama waja wazito, kwani madhara ya kuwa na upungufu mkubwa wa Vitamin D unaweza kusababisha kuzaa mtoto mwenye utindio wa ubongo.

Katika makala yake, Dk. Mercola ameeleza kuwa tangu miaka ya 2000, utafiti kuhusu umuhimu wa Vitamin D umeongezeka sana. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2012, tayari zilikuwa zimeshachapishwa tafiti karibu 34,000 na kuna kumbukumbu (references) za kitabibu zaidi ya 800 ambazo zinaonesha uwezo wa Vitamin D katika kuzia saratani.

Kwa mujibu wa mwanzilishi wa mtandao ujulikanao kama GrassrootsHealth, Bw. Carole Baggerly, kiasi cha asilimia 90 ya saratani ya kawaida ya matiti ina uhusiano mkubwa na upungufu wa Vitamin D mwilini.

Katika jarida la ‘Anticancer Research1’, toleo la Machi mwaka huu, kumechapishwa utafiti wa wagonjwa wa kansa ya matiti waliopimwa kiwango cha Vitamin D. Iligundulika kwamba wenye kiasi kingi cha Vitamin D wana uwezekano wa kupona na kuishi kwa muda mrefu mara mbili ya wale wenye kiwango cha chini cha Vitamin hiyo.

VITAMIN  D  UNAIPATAJE?
Kama nilivyo dokeza kidogo hapo juu, chanzo kikubwa cha Vitamin D ni mwanga wa juu. Utaweza kupata Vitamin D kwa kuota jua, hasa lile la kati ya saa moja asubuhi na saa sita mchana, hata kwa muda wa angalau dakika kumi tu.

Chanzo kingine ni kutumia vidonge vya virutubisho vya Vitamin D vinavyotengenezwa na makampuni yanayoaminika kimataifa.

Hivyo wito wangu kwako msomaji, hakikisha unapigwa na mwanga wa jua kila siku japo kwa dakika chache ili kupata Vitamini hii muhimu kwa kinga ya mwili wako dhidi ya maradhi hatari.


Thursday, May 18, 2017

MBINU ZA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA


Miongoni mwa mambo magumu kabisa katika ufanikishaji wake ni mtu kuachana na uvutaji wa sigara. Watu wengi wamekuwa wakionywa kuachana na uvutaji wa sigara kwa sababu ya madhara yake, lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukolewa na kiwango cha Nikotini inayopatikana katika tumbaku.
Vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji kwa kufuata mkumbo, lakini baadaye wanapokuja kutambua kuwa wako katika hatari ya kuambukizwa au pengine wana ugonjwa wa kifua kikuu, wanakuwa katika wakati mgumu wa kuachana na uvutaji huo. Wengi wao wamekufa huku makundi kwa makundi wakitangatanga kutafuta suluhu ya kuchana na uvutaji, si tu kwa sababu ya kuhofia ugonjwa, bali hata kukosa uwezo wa kununua bidhaa hiyo.
Hata hivyo idadi kubwa ya wanaojaribu kuacha wamejikuta wakipata majibu ya kutoweza, kutokana na kusumbuliwa na hamu ya uvutaji, umbumbu wa mawazo pindi wanapokaa muda mrefu bila kuvuta, kuumwa na kichwa na hata udhaifu katika kukumbuka vitu au mambo waliyofanya au waliyopanga kuyatenda.
Pamoja na yote hayo watalaam na washauri wa masuala uvuaji wa sigara wanasema wanaopatwa na hayo wamekosa mbinu na muongozo wa kuwasaidia waachane na uvutaji wa sigara bila kupata madhara.
Kwa ufupi somo hili limehusisha uchunguzi wa kina pamoja na kumbukumbu za kitaalamu kutoka kwa washauri kama Anderson JE, Jorenby DE, Scott WJ, Fiore MC, Bailey WC, Cohen SJ, ambao wote kwa pamoja kupitia vituo vyao kikiwemo cha US Department of Health and Human Services na Public Health Service walishawahiwa kueleza mbinu salama za kuachana na uvuaji wa sigara. 
Zifuatazo ni dondoo kadhaa za kufuata ili mvutaji aache sigara kwa usalama.

  1. Mvutaji lazima afahamu ni muda gani ambao huwa anavuta sigara kwa wingi, je ni wakati akiwa amelewa au akiwa na mawazo mengi ya kimaisha? Akishafahamu hilo ajiulize ni kiwango gani cha sigara ambacho huwa unavuta kwa siku?
  2. Baada ya hapo achukua kitabu chake cha kumbukumbu na aandike muda huo ambao yeye huvuta sigara kwa wingi. Ajiulize kwa nini huwa unavuta, atathimini madhara ya uvutaji wa sigara kwake binafsi na kwa familia yako.
  3. Kaa chini upitie kwa makini kumbukumbu zako za muda na kiwango cha sigara unazovuta kwa nyakati hizo, kisha panga utaratibu mpya. Kwa mfano kama unavuta sana wakati ukiwa kwenye mawazo hakikisha kuwa unapoanza kufikiria juu ya jambo fulani uwe na kitu mbadala kitachukua nafasi ya sigara. Mfano kahawa au chai? Hakikisha kila penye hamu ya uvutaji unaweka kitu kingine mbadala cha kufanya zaidi ya kuvuta sigara.
  4. Ondoa masalio ya sigara katika sehemu ambazo unaishi, fua nguo zote na vitambaa ili kuondoa harufu ya sigara katika eneo unalokuwepo. Usikae karibu na mtu anayevuta, usikubali kuwa mshirika wa mvutaji na usiwe mtu wa kuendekeza sana msukumo wa mwili unaotaka uvute, bali kila unapowaza juu ya kuvuta fikiria madhara na nia yako ya kuacha.
  5. Wafahamishe rafiki zako kuwa umeamua kuachana na uvutaji, ili upate watu wa kuwaonea aibu pale utakapoanguka na kurudia uvutaji wa sigara. Panga tarehe ya kuacha na iwe kwenye kumbukumbu.
  6. Wakati ukiiendea tarehe hiyo ya kuacha hakikisha unapunguza kiwango cha uvutaji kadiri unavyoisogea siku hiyo. Jipangie muda mrefu zaidi ya kuvuta kulingana na kiwango chako cha uvutaji na kuendelea kuuongeza kila siku ili uzoee kukaa saa nyingi bila kuvuta.
  7. Fuata ratiba mbadala uliyojiwekea kuziba pengo la uvutaji, kama umepanga kutumia kahawa kila unapokuwa mpweke sebuleni hakikisha unajizoeza ili ikifika tarehe yako ya kuacha usiwe mtu wa kujiuliza cha kufanya nyakati ambazo utakuwa na hamu ya sigara.
  8. Lengo lako liwe ni kufanikiwa na usikate tamaa utakaposhindwa kufanikisha lengo lako kwa wakati uliojipangia. Mara kwa mara nenda kamuone daktari mshauri ili akupe muongozo zaidi wa kukusaidia na ikiwezekana akupe nafasi ya kuwatembelea wagonjwa waliopata ugonjwa wa kifua kwa sababu ya kuvuta sigara.
Kwa kifupi hizo ni dondoo chache tu za kukusaidia kuachana na uvutaji wa sigara, lakini mara nyingi kinachoweka nguvu za kufanikisha uachaji wa sigara ni utashi wa mtu ambao hutokana na tathimin ya kina ya muhusika na mtazamo wake juu ya sababu za kuacha. Mara nyingi wanaoshindwa ni wale ambao hawakuzitia nguvu sababu za kuacha kwao.
Siku zote mwanadamu anaongozwa na utashi na kila mwenye kutaka hufanikiwa. Hii ina maana kuwa kama mwanadamu atasema hawezi kuacha kitu fulani, haina maana kama hawezi kwa sababu ameshindwa kujizuia bali ameamua kutokutaka na kinachomshinda ni matokeo ya  maamuzi yake. Kila anayetaka jambo hufanikiwa na hata wavutao sigara wanaweza kuacha kama wakitaka kufanya hivyo.