Mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki na wapenzi wa timu hizo hadi dakika 90 zinakamilika ziliishia 0-0 huku kila timu ikijutia makosa waliyoyafanya Uwanjani.
Akizungumza na gazeti hili jana, Sonso, alisema kuwa walikuwa wamejipanga vyema kushinda mchezo huo lakini makosa waliyoyafanya kipindi cha pili yaliwagharimu.
"Hatukucheza vizuri kipindi cha kwanza, kipindi cha pili tulipata nafasi nyingi lakini tulishindwa kuzitumia, ki ukweli hatuketegemea kudondosha pointi," alisema Sonso.
Alisema kuwa wapinzani wao wajitahidi kucheza vizuri na kuwabana muda wote wa mchezo.
Alisema pia uamuzi wa benchi la ufundi la timu yao kuwapumzisha baadhi ya nyota wao umechangia kushindwa kuibuka na ushindi.
"Unajua wachezaji wengi wamecheza mechi nyingi na wamechoka, makocha waliamua kuwapumzisha baadhi ya wachezaji na hii imechangia kushindwa kupata ushindi," aliongeza kusema Sonso.
Kwa sasa Lipuli ambao msimu ujao wanashiriki ligi kuu ya Tanzania bara wamefikisha pointi 30 na Alhamisi wataelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo dhidi ya Pamba ya mkoani humo.
No comments:
Post a Comment