Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), jijini Mwanza imethibitisha Kampuni ya Korea Kusini kuchukua Kandarasi ya ujenzi wa Meli kubwa katika ziwa Victoria lengo likiwa ni kuboresha huduma ya bandari.
Akizungumza katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 13 ya Usimamizi wa Bandari, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alisema mazingira ya Bandari inazidi kuboreka kutokana na Mji wa Mwanza kuwa Kitovu cha Maziwa Makuu Afrika Mashariki.
"Sisi mikakati yetu kupitia Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk. John Magufuli ni kuhakikisha wananchi wanapata fursa za ajira na biashara ambapo pato litaongezeka katika Halmashauri husika na Serikali Kuu," alisema Mongella.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Bandari mkoani hapa Daniel Sira alisema kuwa bandari hiyo, lengo lake ni kuhudumia kiasi cha mizigo tani milioni moja na abiria milioni moja kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Sira alieleza kuwa mamlaka hiyo ina bandari mbili za nchi kavu, Bandari ya fera ambayo inatarajia kujengwa hivi karibuni na Isaka iliyoko kahama shinyanga.
Meneja huyo alisema wamekuwa karibu na jamii kwa kutoa huduma mbalimbali mashuleni na hosptalini ndani na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa.
No comments:
Post a Comment