Huenda ndivyo walivyozoeleka kuonekana wakisimama hivyo, lakini vipi na kwanini ndege hao husimama kwa mguu moja bado ni kitendawili cha muda mrefu.
Sasa kundi kutoka Marekani limeonyesha kuwa flamingo hawatumii misuli yoyote wanaposimama kwa mguu moja jambo linalomaanisha kuwa hawatumii nguvu.
Ni hali inayowaruhusu kusimama hivyo kwa madaha huku wakisinzia.
Awali watafiti walishangaa iwapo kusimama hivyo kunasaidia kupunguza uchofu wa misuli wakati ndege hao walibadili kutoka kusimama kwa mguu moja hadi jingine.
Makundi ya watafiti wengine yamegundua kuwa hali hii huwasaidia ndege hao kusawazisha ujoto wa mwilini.Sasa profesa Young-Hui Chang, kutoka taasisi ya teknolojia ya Georgia (Georgia Tech) huko Atlanta, na Lena H Ting, wa chuo kikuu cha Emory, wamegundua siri ya mbinu hiyo.
Watafiti hao waliwafanyia uchunguzi kadhaa ndege walio hai na waliofariki. Na wamegundua kuwa Flamingo wanaweza kusimamishwa kwa mguu mmoja pasi usaidizi wowote.
"Unapomtizama ndege huyo usoni, anaposimama kwa mguu moja, mmguu uko chini ya mwili inayomaanisha kuwa mguu umejipinda kwa ndani. Inabidi usimame hivyo iliwa kuweza kuidhinisha mfumo wa kutua," Prof Chang ameiambia BBC.
Hatahivyo, ndege waliokufa hawawezi kusimama kwa miguu miwili, inayomaanisha jukumu kubwa la kutumika misuli katika kiwango hichi.
Watafiti hao pia waliwachunguza ndege walio hai, na kugundua kwamba wanaposimama kwa guu moja na kupumzika hawakusogea hata chembe. Jambo linalothibitisha u thabiti wa kusimama kwa aina hiyo.
No comments:
Post a Comment